Friday, January 06, 2006

Mabaharia watatu kortini kwa kuwatosa Watanzania baharini 2006-01-07 09:04:26 Na Johannesburg, Afrika Kusini
Mabaharia watatu wa Ukraine wamefikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini kujibu mashtaka ya kuwatumbukiza baharini Watanzania waliokuwa wamezamia ndani ya meli yao. Watanzania wawili walikufa maji katika tukio hilo lililokea Jumatano iliyopita karibu na bandari ya Durban. Msemaji wa polisi mjini Durban Bi. Ugu Sabela alisema mabaharia hao na nahodha wa meli hiyo walifikishwa mahakamani jana. Alisema hata hivyo wameachiwa kwa dhamana ya dola 3,200 za Kimarekani. Bi. Sabela alisema kutoswa kwa Watanzania hao baharini kulikuja baada ya meli hiyo kuwasili mjini hapa ikitokea Mombasa nchini Kenya. Sheria za Afrika Kusini zinawataka wenye meli zilizowabeba wazamiaji kulipa gharama za kuwarejesha nchini mwao. Wazamiaji watano miongoni mwa saba waliweza kuogelea lakini wengine wawili walishinda na hatimaye kufa maji. Msemaji wa polisi alisema mabahari hao kila mmoja anashtakiwa kwa makosa mawili ya kuua na matano ya kujaribu kuua. Kwa upande wake nahodha anakabiliwa na mashtaka ya kusaidia kuwasafirisha wahamiaji haramu na kwamba kuna uwezekano pia wa kukabiliwa na mashtaka kuua na kujaribu kuuwa. Habari zilisema waokoaji bado hawajafanikiwa kuzipata maiti za Watanzania wawili walitoswa baharini. Polisi nchini Afrika Kusini, imesema tatizo la vijana kuzamia linazidi kuwa kubwa.

3 Comments:

Blogger Ndesanjo Macha said...

Ndio Silvery, njia iko wazi. Kazi ni kwako. Karibu.

11:55 AM  
Blogger Ndesanjo Macha said...

Ukiwa na maswali zaidi usisite kuuliza. Uliza mwanablogu yeyote maana mtandao wetu umejengwa juu ya falsafa ya ujamaa.

11:56 AM  
Blogger FOSEWERD Initiatives said...

silver, nimefurahi kwa kuweka habari hii ya kijana kuzamia afrika kusini. umenirudisha kwenye makala moja za mwandani au harakati kuwa tatizo kubwa la kwetu hasa watanzania ni kuamini kuwa namna tunavyoyachukulia mambo ndio sahihi na tuko vizuri kuliko mataifa mengi ulimwenguni ambayo yenyewe yaliamua kukuza demokrasia yao kwa ajili ya maendeleo. pia huwa tunachukia kuelezwa ukweli na kuwaona walio ughaibuni kuwa ni maadui wa taifa letu. narudi kwa hao vijana. kama nchi yetu ingekuwa ina ahueni, mbona bado watu wanazamia meli na kurisk kutupwa majini? mbona wanabeba unga? kuna kazi ya kufanya hapo

4:51 AM  

Post a Comment

<< Home